Iran imekanusha mazungumzo ya siri kati ya balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa na Elon Musk ili kupunguza mvutano kati yake na Marekani, miezi miwili kabla ya Rais mpya wa Marekani Donald Trump kuchukua madaraka
Hakukuwa na mkutano.
Huu sio wakati wala kwa maslahi yetu.
Tunasubiri kusikia msimamo wa utawala wa Rais Donald Trump.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran.
Hata hivyo, mashaka bado yapo juu ya uwezekano wa mkutano kati ya pande hizo mbili, anaripoti mwandishi wetu hukoTehran, Siavosh Ghazi.
Gazeti la New York Times, likinukuu vyanzo vya Iran ambavyo havikujulikana majina, lilitaja mkutano wa Novemba 11 huko New York kati ya bilionea Elon Musk na balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Amir Saeid Iravani.
Vyanzo vilivyonukuliwa na gazeti hili vilieleza kuwa mkutano huo wa zaidi ya saa moja ulikuwa “chanya” na ulionyesha “habari njema”.