Top Stories

Iran yapiga marufuku chanjo kutoka Marekani na Uingereza

on

Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amepiga marufuku uingizaji wa chanjo ya Covid-19 kutoka kampuni ya Pfizer ya Marekani na mshirika wake BionTech, sambamba na chanjo ya Uingereza ya Astrazeneca kwa kile alichokitaja kama kukosa imani na mataifa ya Magharibi.

Katika hotuba kupitia vyombo vya habari Khamenei amesema Iran haitoagiza chanjo za Marekani na Uingereza akiashiria idadi ya vifo vinavyoendelea kusajiliwa katika mataifa hayo.

Aidha kiongozi huyo amedai kwamba mara nyingine mataifa hayo yamekuwa yakitaka kufanya majaribio ya chanjo zao kwa watu wa mataifa mengine akiijumuisha pia na Ufaransa.

Kiongozi huyo amekubali kuingizwa kwa chanjo kutoka mataifa mengine salama na anaendelea kuunga mkono juhudi za Iran kutengezeneza chanjo yake ambayo tayari inafanyiwa majaribio tangu mwezi Disemba na inatarajiwa kuanza kuuzwa kufikia majira ya machipuko.

SVEN AFUNGUKA YA MOYONI “MOYO MZITO, MO DEWJI ALITAKA NIBAKI”, KOCHA PAKA, REKODI ZAKE ZA KIBINGWA

Soma na hizi

Tupia Comments