Top Stories

Iran yasisitiza italipa kisasi kifo cha Soleimani

on

Kiongozi wa Hezbollah, Hassan Nasrallah amesema kutakuwa na operesheni mbalimbali dhidi ya Vikosi vya Marekani katika Kanda ya Mashariki ya Kati ili kulipiza kisasi Marekani kwa kuwaua Makamanda wa Iran na Iraq.

Nasrallah ameyasema hayo katika hotuba yake ya kukumbuka wiki moja ya kifo cha Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Iran, Qasem Soleimani na Kamanda wa Wanamgambo wa Iraq, Abu Mahdi al-Muhandis.

Amesema, Marekani haina chaguo lingine ila kuwaondoa wanajeshi wake kwa hiari au kurudisha miili yao ikiwa katika majeneza.

Aidha, amekanusha madai ya Rais Donald Trump kuhusu Soleimani kuwa na mipango ya kushambulia Ubalozi wa Marekani.

ASKARI AKUSANYA ZAIDI YA LAKI SABA KUSAIDIA KITUO KILICHOANZISHWA NA MTOTO WA MTAANI

Soma na hizi

Tupia Comments