Mamlaka ya mahakama ya Jamhuri ya Kiislamu imewanyonga wafungwa wengine wanane katika jela mbalimbali za Tabriz, Isfahan, Birjand na Zahedan, kwa mujibu wa ripoti kutoka mashirika ya kutetea haki za binadamu kulingana na VOA.
Katika wiki za hivi karibuni, maafisa wa Umoja wa Mataifa, mawakili wa wafungwa na wengine wametoa taarifa kwa mnasaba wa Siku ya Kupinga Adhabu ya Kifo Duniani, wakielezea wasiwasi wao juu ya kuongezeka kwa idadi ya watu wanaonyongwa nchini Iran na kutaka kusitishwa mara moja.
Kwa mujibu wa Amnesty International, Jamhuri ya Kiislamu iliwajibika kwa asilimia 74 ya mauaji ya watu wote duniani mwaka 2023.