Kundi la Islamic Resistance in Iraq (IRI) ambalo ni muungano wa mirengo, limedai kuhusika na mashambulizi matano ya ndege zisizo na rubani katika maeneo ya kijeshi nchini Israel.
IRI ilitangaza mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kaskazini na kusini mwa Israel katika mfululizo wa sasisho kwenye Telegram.
Ilisema hatua zake ni “kuunga mkono watu wetu huko Palestina na Lebanon, na kukabiliana na mauaji yaliyofanywa na shirika la uporaji dhidi ya raia, wakiwemo watoto, wanawake na wazee”.
Hapo awali, jeshi la Israel lilisema jeshi lake la anga lilinasa ndege nne zisizo na rubani “kutoka mashariki” usiku kucha.