Duniani

Baada ya miaka 40 kupita, huyu ndio mrembo wa kwanza kuvaa Taji la Miss Iraq..

on

December 19 2015 warembo kutoka nchi zaidi ya 100 duniani walikutana Sanya China kwenye stage moja wakishiriki kugombea Taji la Miss World, bahati nzuri ikawa kwa watu wa Spain, mrembo wao Mireia Lalaguna Rozo akaibuka na ushindi wa Taji hilo.

Stori ikafatia usiku wa December 20 2015 kutoka Las Vegas Marekani ambapo fainali za Miss Universe zimefanyika, mrembo kutoka Ufilipino, Pia Alonzo Wurtzbach nae kafanikiwa kuibuka na ushindi wa Taji hilo.

Wakati stori zikiendelea hivyo unajua kilichokuwa kinaendelea Iraq ??!! Labda wengi tumesikia taarifa kuhusu migogoro, machafuko na vita… masuala ya urembo je ??

IRAQ

Miss Iraq 2015, mrembo Shaima Qassim

Taarifa ikufikie kwamba kwa mara ya mwisho mashindano ya urembo Iraq yamefanyika mwaka 1972 na tangu wakati huo hayajafanyika tena mpaka hii leo ambapo nimekutana na stori ya mashindano ya Miss Iraq yamefanyika na mrembo Shaima Qassim ameibuka mshindi wa mashindano hayo baada ya miaka zaidi ya 40 kupita bila Iraq kuwa na mashindano ya urembo.

Video yake hii hapa, lugha wanayozungumza ni kiarabu lakini unaweza kuona alivyovalishwa Taji.

https://www.youtube.com/watch?v=ioQkEfBcLFE

Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye TwitterFBInstagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>> INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Soma na hizi

Tupia Comments