Mix

Hii ni kuhusu Magari mawili yaliyowaka moto Iringa leo.

on

IMG_9803+-+CopyMkoani Iringa leo basi moja lanusurika  kuwaka  moto na daladala  moja  yateketea yote kwa moto  wakati  wanafunzi wa masomo ya  kuunga vyuma katika gereji  bubu  eneo la uwanja  wa  Samora  mjini  Iringa  wakijifunza kuunga ngao  ya  daladala  hiyo yenye  namba za  usajili T189 AWN .
IMG_9802+-+CopyTukio  hilo  limetokea  leo majira ya 8 na dakika 15 mchana  wakati  vijana  wawili wanaojifunza  kuunga vyuma wakiendelea na  mafunzo ya  kuunga  ngao ya  daladala  hilo.

Mmoja kati ya  wafanyakazi wa gereji  hiyo Filibert Mwihava  amesema  kuwa chanzo  cha  daladala  hilo  kuwaka  moto ni  vijana  wawili ambao  wanajifunza  ufundi  wa  kuunga  vyuma katika eneo hilo kufanya  kazi  hiyo  bila kuzingatia kanuni ya kazi hiyo.

 IMG_9798+-+CopyKanuni hizo ambazo  vijana hao walikosea amezitaja kuwa ni pamoja na  kuunga ngao ya nyuma ya  daladala  hilo wakiwa jirani na tenki la mafuta  hivyo kutokana na cheche  zilizokuwa  zikitoka  zilisababisha moto kuibuka kwa kasi .
IMG_9794Mwihava  amesema katika moto  huo kushika daladala  hiyo inayofanya  safari  zake kati ya  Tumaini na Zizi la Ng’ombe  mjini  Iringa hakuna mtu  aliyezulika  zaidi ya  basi  lenye namba za  usajili T 457 AMQ kutetekea  upande wa  mbele  kabla ya  kuokolewa .
Kikosi cha  zimamoto  na uokoaji mkoani Iringa  walifika kwa  wakati na kufanikiwa  kuzima moto  huo ambao pengine ungeweza  kusababisha  madhara  makubwa katika  eneo hilo lenye  ofisi ,maduka ya watu  waliojenga  kuzunguka uwanja  huo wa  Samora.
IMG_9797Akithibitisha  kutokea  kwa  tukio  hilo kiongozi  wa askari wa zimamoto  ambao  walifika  eneo hilo John Zacharia  amesema  kuwa  kuwa  chanzo cha moto  huo ni uzembe wa ofisi  hiyo.
Source:http:www.matukiodaima.com

Tupia Comments