Isaac Mnyagi mkazi wa kata ya Sombetini Katika jiji la Arusha amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha amesomewa shtaka la shamulio la kumdhuru mwili wa mke wake Jackline Mkonyi kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake pamoja nakumng’oa jino kwa kifaa cha nchakali.
Mbele ya Hakimu,Jenifa Edward wa mahakama ya Wilaya ya Arusha,katika kesi namba 80 ya mwaka 2023, wakili wa serikali Charles Kagilwa akisaidiana na Godfrey Nungu na Callorine Kasubi,alidai mnamo Mei 23 mwaka huu majira ya saa tano usiku katika eneo la Osunyai kwa Diwani jijini Arusha Mshtakiwa Mnyangi alimshambulia Jackline Mkonyi(38)ambaye ni mke wake na kumng’oa jino moja ,kumpiga kwa Mkanda Usoni na mgongoni na maeneo ya mwili wake na kimsababishia madhara.