Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema suala la bando za simu kuisha muda wake sio wizi kwa Watumiaji bali ni utaratibu wa kawaida kabisa wa kibiashara.
Waziri Nape amesema hayo leo November 10, 2022 wakati akifafanua hoja iliyoibuliwa na Mbunge wa Jimbo la Mkalama, Francis Isack Mtinga aliyedai kuwa Kampuni zimekuwa zikiwaibia Watumiaji wa simu kwa kuwa bando zimekuwa zikiisha muda wake hata kabla hazijamalizika.
“Bando ni huduma ya ziada ambayo ina masharti ya muda ndio maana kuna bando la wiki, mwezi na kuendelea na ukitaka lisiishe kwa muda uko utaratibu wa kutumia main tarrif hata kama utakaa nao mwaka mzima”.