Stori Kubwa

Jinsi Mtangazaji Kibonde na Producer Sheddy walivyokumbwa na ishu ya ‘Panya Road’ Dar Jan 2 2015

on

.Stori ambayo imechukua nafasi kubwa ya kujadiliwa kuanzia mida ya jioni Dar es salaam ni kuhusu kikundi cha wezi wanaotumia ubabe maarufu kama Panya Road ambacho kinaaminika kuvamia maeneo kadhaa ya Dar es Salaam ikiwemo Sinza, Mwananyamala, Tabata na sehemu nyingine.

Taarifa ambazo zilianza kusambaa kutoka kwa mashuhuda ni kwamba Wezi hawa walikua wakipiga watu, kupora vitu mbalimbali na hata kuharibu baadhi ya magari na pikipiki kwa kuvunja taa wakati wakipita kwenye mitaa mbalimbali.

Baada ya taarifa kusambaa Kamanda wa Polisi kanda maalum ya Dar es salaam Suleiman Kova alizungumza kwenye TBC1 na kusema hawezi kupinga uhalifu kufanyika leo mtaani lakini sio kwa kiasi hicho ambavyo imeripotiwa, yaani habari imekuzwa kuliko ukweli wenyewe.

Miongoni mwa waliothibitisha tukio la magari kuvunjwa taa na wenye magari kuyaacha kandokando ya barabara magari hayo ni producer wa bongofleva Sheddy Clever alietengeneza hits kama ‘number one‘ ya Diamond Platnumz.

Mwingine aliekumbwa na huu mkasa ni mtangazaji wa Clouds FM Efphraim Kibonde kama ambavyo wote wanasikika wakizungumza kwenye hizi sauti hapa chini.

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta Facebook

Tupia Comments