Ripoti ya shirika la habari la AFP, ikinukuu vyanzo viwili vinavyofahamu mazungumzo hayo, ilisema kuwa makubaliano hayo ya muda ni pamoja na usitishaji vita wa siku tano, unaojumuisha usitishaji mapigano ardhini na mipaka kwa operesheni za anga za Israel kusini mwa Gaza.
Kwa kubadilishana na kurejeshwa kwa wafungwa kati ya 50 na 100 wanaoshikiliwa na Hamas na Islamic Jihad, ambayo itajumuisha raia wa Israeli na mateka wa mataifa mengine, lakini sio wanajeshi.
Sehemu ya makubaliano hayo inaweza kujumuisha kubadilishana wanawake na watoto wa Kipalestina waliozuiliwa nchini Israel kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas, ripoti hizo zimeongeza.
Iwapo itakubaliwa, baadhi ya Wapalestina 300 pia wataachiliwa kutoka jela za Israel, miongoni mwao wakiwa wanawake na watoto.