Israel imeahidi hivi punde siku ya Alhamisi, Septemba 26 kupambana na Hezbollah kutoka Lebanoni “hadi ushindi”, ikikataa wito wa kimataifa wa kusitisha mapigano kwa siku 21, huku mashambulizi makubwa ya anga yakiendelea mashariki na kusini mwa Lebanoni.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amebaini kuwa itakuwa “kosa” kwa Benjamin Netanyahu kukataa usitishaji mapigano.
Katika mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku ya Jumatano Septemba 25, Ufaransa, Marekani na nchi nyingine za Ulaya na Kiarabu zilitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano kwa muda kwa siku 21 kati ya Israel na Hezbollah. Pendekezo ambalo lilikataliwa haraka na Israeli.
“Hili ni pendekezo la Marekani na Ufaransa ambalo Waziri Mkuu hata hajajibu,” imesema taarifa kutoka ofisi ya Netanyahu, na kuongeza kuwa Waziri Mkuu wa Israeli ameagiza jeshi “kuendeleza mapambano kwa nguvu zote zinazohitajika.
Jeshi la Israel limebainisha kuwa linajiandaa kwa “kuingia kunakowezekana” kwenye ardhi ya Lebanoni ili kushambulia Hezbollah.