Israel ilisema inatuma timu ya kufanya mazungumzo ya awamu inayofuata ya usitishaji vita dhaifu na Hamas, ikiashiria maendeleo yanayowezekana kabla ya mkutano wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na Rais wa Marekani Donald Trump.
Netanyahu atakuwa kiongozi wa kwanza wa kigeni kukutana na Trump katika Ikulu ya White House tangu arejee mamlakani mwezi uliopita, na kuna uwezekano atakabiliwa na shinikizo la kuheshimu usitishaji vita ambao kiongozi huyo wa Marekani amedai kusitisha.
Saa chache kabla ya mkutano wao, ofisi ya Netanyahu ilisema Israel itatuma ujumbe katika mji mkuu wa Qatar Doha baadaye wiki hii kwa mazungumzo.
Hamas imesema iko tayari kujadili hatua ya pili ya usitishaji vita, inayopatanishwa na Qatar, Marekani na Misri, na ambayo inapaswa kuzingatia kusitishwa kwa kudumu zaidi kwa vita.