Makubaliano ya kusitisha mapigano kati ya vikosi vya Israel na kundi la wanamgambo wa Lebanon Hezbollah yalianza kutekelezwa Jumatano asubuhi saa za huko, kwa mujibu wa ratiba iliyowekwa na Rais wa Marekani Joe Biden, baada ya Israel na Lebanon kukubaliana makubaliano ya kumaliza mzozo huo uliodumu zaidi ya mwaka mmoja.
Akizungumza hapo awali katika bustani ya White House Rose, Biden alisema mpango huo “umebuniwa kuwa usitishaji wa kudumu wa uhasama.”
Alisema amezungumza na viongozi wa Israel na Lebanon, na kwamba nchi zote mbili zilikubali pendekezo la Marekani “kumaliza mzozo mbaya” kati ya Israel na Hezbollah.
Baraza la mawaziri la usalama la Israel lilipiga kura siku ya Jumanne kuidhinisha makubaliano hayo kwa wingi wa 10 kwa mmoja, ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel ilisema, ikishukuru Marekani kwa kuhusika kwake.