Maafisa wa Israel na Palestina wamekubaliana kusitisha mapigano baada ya mazungumzo ya nadra nchini Jordan, hii ni baada ya kuongezeka kwa machafuko mwaka huu na kusaababisha Waisraeli wawili kuuawa katika Ukingo wa Magharibi wakati mkutano ukiendelea.
Katika taarifa yao ya pamoja baada ya mkutano huo uliofanyika eneo la Pwani la Aqaba pande zote zimekubaliana kuachana na hali ya kuhasimiana na kujitenga na machafuko zaidi.
Wakati mazungumzo hayo yakiendelea, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu na waziri wake wa usalama wa taifa, Itamar Ben-Gvir, walisema katika taarifa kwamba “raia wawili wa Israel waliuawa katika shambulio la kigaidi la Wapalestina” eneo ambalo Israel inalikalia kimabavu tangu kufanyika kwa Vita vya Siku Sita vya mwaka 1967
muendelezo wa hatua hiyo wajumbe hao wataendelea na mazungumzo yanayojikita katika kujadili njia za kutuliza mivutano ya kiusalama katika eneo hilo kabla ya mwezi wa Ramadhani”, ambao unaanza katika kipindi kifupi kijacho.