Israel inasema imewakamata wanachama 200 wa makundi ya Hamas na Islamic Jihad katika muda wa wiki moja iliyopita na kuwapeleka katika eneo lake kwa mahojiano.
Taarifa ilisema baadhi ya washukiwa hao walikuwa wamejificha miongoni mwa raia na kujisalimisha kwa hiari.
Israel inasema wanamgambo 700 wa Kipalestina wametiwa mbaroni tangu ilipoanzisha operesheni yake ya kijeshi na uvamizi wa Gaza kwa lengo la kuwatokomeza Hamas.
Hamas inasema wanawake na watoto wanauawa sana na Waisraeli.
BBC haijafanikiwa kuthibitisha madai hayo.
Israel ilianza operesheni yake ya kulipiza kisasi baada ya wapiganaji wa Hamas kuvuka kutoka Gaza hadi kusini mwa Israel tarehe 7 Oktoba, na kuua watu 1,200 na kuchukua mateka wapatao 240.
Takriban watu 20,000 wameuawa na 50,000 kujeruhiwa huko Gaza tangu wakati huo, kulingana na wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas.
Israel imeendeleza kampeni yake ya kulipua mabomu huko Gaza – kuwaamuru raia kuondoka