Wanaharakati nchini Israel wamemtaka Netanyahu kukubaliana na makubaliano ya kusitisha mapigano na kubadilishana mateka na wafungwa, lakini wanalalamika kuwa badala yake amezuia kwa makusudi mpango wowote unaowezekana.
Wengi wanadai kwamba anataka kurefusha vita kwa ajili ya uhai wake wa kisiasa, akishikilia maslahi yake mwenyewe juu ya yale ya nchi.
Kundi la wapiganaji wa Palestina Hamas lilisema Jumatatu kwamba mateka 33 wa Israel wanaoshikiliwa huko Gaza wameuawa, hasa kutokana na mashambulizi ya anga ya Israel tangu Oktoba 7, 2023.
Katika video iliyotumwa kwenye Telegram, kundi la upinzani lilisema: “Mateka 33 wa Israel waliuawa, na baadhi ya maeneo yao hayajulikani waliko kwa sababu ya hatua na ukaidi wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu.”
Kundi hilo lilionya kuwa kuendelea kwa uchokozi wa Israel kutaongeza idadi ya vifo miongoni mwa mateka wa Israel.
Israel imewateka nyara zaidi ya Wapalestina 10,100 wanaoendelea kuteseka katika jela na vyumba vya mateso.