Jeshi la Israel lilizuia lori za mafuta kufika hospitalini kaskazini mwa Ukanda wa Gaza huku kukiwa na mashambulizi ya kijeshi katika eneo hilo, mamlaka za eneo zilisema jana.
Jeshi la Israel liliendelea na mashambulizi ya kijeshi kaskazini mwa Ukanda wa Gaza kwa siku ya tano jana huku kukiwa na mzingiro mkali katika eneo hilo, kwa mujibu wa mashahidi.
Jeshi la uvamizi liliamuru hospitali tatu kuhama ndani ya masaa 24 kama sehemu ya uvamizi unaoendelea.
“Jeshi la Israel limezuia usambazaji wa mafuta ya dizeli katika hospitali kaskazini mwa Gaza kwa mara ya tano mfululizo,” Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Serikali ya Gaza ilisema.
“Hospitali zote na vituo vya matibabu viko katika hatari ya kufungwa ndani ya masaa 24,” ilionya katika taarifa, na kuongeza kuwa huu ni “uhalifu uliopangwa kikamilifu” unaolenga kudhoofisha mfumo wa afya kaskazini mwa Gaza, ambapo watu 700,000 wanaishi.