Premier Bet
TMDA Ad

Habari za Mastaa

BEEF: Timbulo kuhusu kuibiwa wimbo na Abdukiba ‘wametaka niwaongelee’

on

Baada ya msanii Abdukiba kutoa wimbo wake mpya kumekuwepo maneno kuwa Abdukiba kamuibia msanii Timbulo wimbo huo ambapo Ayo TV entertainment ikamtafuta Timbulo kwenye Exclusive Interview ili kufahamu ukweli wa hilo jambo ukoje.

Timbulo amezungumza na kusema kuwa ni kweli wimbo alioutoa Abdukiba yeye anahusika nao japo haukuwa wake kama watu wanavyosema bali alishirikishwa na Msanii aliyempa wimbo huo Abdukiba kwani yeye ndiye aliyekuwa wa kwanza kushirikishwa na akatumia gharama zake lakini anashangaa kuona sahivi kapewa Abdukiba na kautoa..

“Nilikaa kimya ila naona maneno yanazidi kutengenezwa nikasema na mimi ngoja niseme ukweli, ila nilisikia kwenye interview kuwa wanasema wimbo ni wa Abdukiba na waliufanya tangia mwaka jana mwezi wa nne kitu ambacho sikweli.” – TIMBULO

Tazama VIDEO kwa kubonyeza PLAY hapa chini kumsikiliza Timbulo akielezea..

Ferouz “Mgahawa wangu ulidumu kwa mwaka mmoja”

Soma na hizi

Tupia Comments