Meli ya MV. Amani kutokea Congo kwa mara ya kwanza imewasili katika Bandari ya Kigoma, kupitia Ziwa Tanganyika meli hiyo imekuja Kigoma kwa majaribio ya kwanza ya safari zake zinazotarajiwa kuanza mwezi ujao kati ya Congo, Burundi, Kigoma na Zambia.
Pia Meli hiyo imelenga kuimarisha biashara katika ya Tanzania, Congo pamoja na Burundi na Nchi zinazunguka Ziwa Tanganyika katika kukuza uchumi zaidi katika biashara katika Ukanda wa Ziwa Tanganyika ambao walikuwa na uhitaji wa meli za mizigo na abiria.
Mkurugenzi wa MV. Amani Solomoni Nansuma amesema meli hiyo imekuja kufungua biashara katika ukanda wa Ziwa Tanganyika na Kampuni hiyo itatoa ajira kwa vijana Mkoani Kigoma kwakuwa wanampango wa kufungua Ofisi Kigoma.
ina uwezo wakubeba abiria zaidi ya 600, vyumba zaidi ya 22 vya kulala vyenye ubora na vya kisasa, uwezo wa kubeba mizigo zaidi ya tani elfu 3500, magari zaidi ya 50, inaenda kwa spidi ya haraka ndiyo meli kubwa katika Ziwa Tanganyika na inatumia Saa 4 kufika Congo.