Mix

Haya ni maajabu ya pete ya kuokota yanayomtokea huyu !

on

ring_sakawaKijana mmoja kutoka Ghana huenda akakatwa kidole chake baada ya pete aliyoiokota na kuivaa kung’ang’ania kwenye kidole ambacho kimeanza kupuputika huku nyama za kidole hicho zikionekana kulika.

Kijana huyo Eric Buageng, alisema iliiokota pete hiyo pembeni ya barabara wakati akirudi nyumbani akitokea Kanisani na kuivaa kwenye kidole chake, akaanza kusikia maumivu na pete hiyo ikaanza kumbana kidole.

Eric-Buabeng

Eric Buageng

Eric amesema kilichomshangaza zaidi ni wakati alipokuwa anaiokota mkono wake ulikuwa ukitetemeka, akashindwa kuitupa pia, halafu akasikia sauti ambayo hakujua ilipotokea ikimwambia aende nyumbani, alipofika alijaribu kuitoa lakini hakuweza na kuna wakati anasikia sauti ikimwambia atoke nje.

Jitihada zake zimeonekana kutokuwa na matumaini yoyote kwenye mikasa inayomkuta kwenye pete hiyo, ameshaenda Hospitali  na pia kwa wachungaji na hakuna mafanikio yoyote huku wakihisi kwamba pete hiyo ina uhusiano na masuala ya uchawi.

filesHautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments