Top Stories

Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Bill Gates IKULU leo

on

Rais Magufuli leo August 10, 2017 amekutana na Mwasisi mwenza wa Taasisi ya Bill and Mellinda Gates Ikulu Dar es Salaam ambaye kupitia Taasisi hiyo ametenga Dola za Marekani Milioni 350 ambazo ni Tsh. Bilioni 777.084 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali katika sekta za Kilimo, Afya na Mifumo ya kielektroniki ya upatikanaji wa taarifa.

Bill Gates amesema kama ambavyo Taasisi yake imeshirikiana na Tanzania kwa kiasi kikubwa katika kuimarisha huduma za afya ambapo fedha hizo zitaelekezwa katika utekelezaji wa miradi zaidi ya afya ikiwemo kupunguza vifo vya uzazi, kukabiliana na ugonjwa wa malaria, kuimarisha lishe na kukabiliana na utapiamlo.

Aidha, zitaelekezwa pia katika sekta ya kilimo ambako zitasaidia kuongeza uzalishaji wa mazao, kuzalisha mbegu bora na kuboresha ufugaji utakaoongeza chakula na pia zitasaidia kuweka mifumo ya kisasa ya upatikanaji wa taarifa.

Rais Magufuli amemshukuru Bill Gates kwa mchango mkubwa unaotolewa na Taasisi ya Bill and Mellinda Gates katika miradi mbalimbali hapa nchini ikiwemo fedha ambazo taasisi hiyo itazito katika kipindi cha miaka mitano kuanzia sasa na amemhakikishia kuwa Serikali yake itahakikisha fedha hizo zinaleta matokeo yaliyokusudiwa.

“Wakizuia maziwa yetu kwao na sisi tuzuie yao siku hiyohiyo” – JPM 

MAGUFULI AFUNGUKA! NI KUHUSU KUTAWALA MIAKA 20 

Soma na hizi

Tupia Comments