AyoTV

VIDEO: Kocha wa Simba SC kajibu kwa jazba “Najua sitaadhibiwa marefa sita!!”

on

Baada ya mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Simba SC kumalizika wakicheza dhidi ya Azam FC katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam kwa ushindi wa 4-2, kocha mkuu wa Simba SC Patrick Aussems aliongea na waandishi wa habari na kueleza kukasirika kwake kuhusiana na waamuzi wa mchezo huo.

Aussems ameoneshwa kushangaza na kuwatuhumu waamuzi kuwa wamekosa umakini, licha ya kuchezesha marefa sita katika mchezo huo, kitu ambacho hakijazoeleka na anaamini kutokuwa kwao makini ndio kumesababisha Azam FC kufunga goli wakati Kapombe kaumia.

“Natumai sitaadhibiwa walikuwa marefa sita, unaweza kuamini? angalia kosa lililofanyika kwa Kapombe ilitakiwa kuwa faulo inayotakiwa kutolewa adhabu ya kadi ya njano”>>>>Aussems

VIDEO: MWALIMU KASHASHA KATOA TATHMINI KWA YANGA HII DHIDI YA TOWNSHIP ROLLERS

Soma na hizi

Tupia Comments