Kuelekea game ya Liverpool dhidi ya Man United itakayochezwa katika uwanja wa Old Trafford, Jumapili ya February 24 2019, kocha wa Liverpool Jurgen Klopp ametangaza taarifa za kuhuisiana na hali ya staa wake Alex Oxlade Chamberlain ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa majeruhi kwa muda mrefu.
Klopp ametanja kuwa hali ya staa huyo imeaimarika kwa kiasi kikubwa na ameanza mazoezi japokuwa bado hayupo fiti kucheza kama ambavyo wachezaji wenginge walivyo katika kikosi chake, kwamba wapo fiti kwa asilimia 100.
“Hatuhitaji kuzungumza kuhusiana na Chamberlain kwa sasa kwa sababu anahitaji muda kidogo kurejea uwanjani, anaonekana kuwa fiti mazoezini lakini tunahitaji kumuangalia zaidi kabla ya kumtumia, Rhian Brewster bado hajawa fiki kuwa katika kundi la wachezaji wanaofanya mazoezi lakini Chamberlain yeye tayari amekuwa akishiriki mazoezi kwa kiasi kikubwa”>>> Chamberlain
Liverpool anakutana na Man United katika mchezo wa Ligi Kuu England Jumapili ya February 24 wakiwa wanahitaji point tatu kurudi kileleni baada ya kufungana point na Man City wanaoongoza kwa kuwa na point 65 na wameizidi Liverpool mchezo wakati Man United wao wanahitaji ushindi kuendelea kusalia nafasi ya nne ili wafikishe point 54 ambazo hata Arsenal akishinda hawezi kuwafikia wataendelea kuwazidi point moja.
Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake