Mshambuliaji wa Brentford Ivan Toney (27) Raia wa England leo amekutwa na hatia ya kujihusisha na masuala ya betting kinyume na sheria za chama cha soka England FA, Toney amefungiwa kujihusisha na soka kwa miezi 8 pamoja na faini ya pound 50,000 (Tsh milioni 147).
Ivan Toney amekutwa na hatia kwa kuvunja sheria namba E8 ya FA kuhusu masuala ya betting ambayo ni kushiriki kubet au kutoa taarifa kwa madhumuni ya betting.
Makosa 232 ya Ivan Toney inadaiwa kuwa alitenda kati ya kipindi cha mwaka 2017-2021 na sasa atakuwa nje ya uwanja akiwa hawezi kuichezea club yake au timu yake ya Taifa ya England hadi January 16 2024.