Michezo

Ivanovic akwepa adhabu ya FA.

on

chelseaeverton

 

Beki wa Chelsea ambaye ni raia wa Serbia Branislav Ivanovic hatakutana na adhabu yoyote ile baada ya kuonekana akimng’ata mchezaji wa Everton wakati timu hizo zilipokutana hapo jana (jumatano) katika mchezo wa ligi kuu ya England .

Picha za Mnato na za magazeti zimeonyesha kuwa Ivanovic alionekana kama amelenga meno yake kwenye bega la mchezaji wa Everton James McCarthy katika dakika ya 86 ya mchezo baina ya timu hizo mbili uliopigwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge .

Picha zilimuonyesha Ivanovic akiwa anaelekea kumng'ata kiungo wa Everton James McCarthy.

Picha zilimuonyesha Ivanovic akiwa anaelekea kumng’ata kiungo wa Everton James McCarthy.

Katika taarifa iliyonukuliwa toka kwenye mtandao wa Chelsea na kwenye mtandao wa chama cha soka cha England Fa , Ivanovic hatakutana na adhabu yoyote ya kinidhamu toka kwa chama hicho kutokana na uchunguzi uliofanywa .

Hata hivyo klabu hizi mbili za Chelsea na Everton huenda zikatozwa faini baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kushindwa kuwazuia wachezaji wa timu zote mbili kuzusha zogo baada ya vurugu zilizowahusisha wachezaji wa timu zote kutokea .

Katika mechi za ligi ya England tukio lolote ambalo halijaonekana na mwamuzi huchunguzwa na jopo huru la watu watatu ambao wana jukumu la kutazama tukio lote na kuishauri Fa juu ya hatua za kuchukuliwa .

Tupia Comments