Golkipa mkongwe aliyewahi kucheza katika klabu za Yanga na Simba Ivo Mapunda August 18 2015 amezungumzia kilichotokea kati yake na Simba mpaka kutopata nafasi ya kuongezewa mkataba kuichezea club hiyo…….. ni kupitia hii Exclusive Interview na millardayo.com
Mwishoni mwa wiki iliyopita Rais wa Simba Evance Aveva alisema Ivo aliitiwa mkataba mpya na klabu ya Simba lakini hakuokea kwenye kuweka saini, ni kama alikua anakwepa hivi…. ikiashiria kwamba kama angekwenda kusaini mkataba mpya siku yoyote kabla ya August 17 kabla hazijaanza kuenea stori kwamba Simba imemtema.
Ivo anafafanua hapa pia kuhusu zile milioni 10 ambazo imesambaa kwamba anadaiwa na Club hiyo ambazo alizichukua kama mkopo.
Ivo Mapunda ameanza kwa kusema >>> “Ni maneno unajua suala la pesa ni suala la siri kati yangu na klabu ila haya maneno ya kuwa nimepokea milioni 8 ni maneno tu ila ni kweli mimi nimepokea pesa kutoka kwa viongozi wa klabu ya Simba ila hizi fununu nyingine zinakuwa sio za kweli’
MTAZAME KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI
Kuhusu Mkataba kusitishwa na Simba: Ivo amesema >>> ‘Nadhani kilichokua kinakwamisha labda ni mawasiliano kati yangu na aliyepewa jukumu la kunitafuta ili nisaini mkataba mpya, huenda hakufanya kazi yake kwa usahihi…. mimi nilikua mgonjwa nikaondoka kambini ghafla Tanga nikarudi Dar kutibiwa, alipeleka taarifa kwamba nimegoma kusaini fomu nimempiga chenga hivyo Mkataba ukasitishwa, mpira una mambo mengi‘
‘Nimekwenda juzi ofisini, Ijumaa nikaenda tena na Jumatatu jana wakasema watanipa majibu….. majibu waliyonipa ni kwamba hawawezi kuendelea na mkataba na mimi….. inaonyesha kabisa kwamba huenda hawakuwa na nia na mimi manake bado muda upo ili kufunga dirisha la usajili“>>> Ivo Mapunda
PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos