Michezo

Majibu ya Ivo Mapunda kuhusu taulo lake jeupe linalo husishwa na imani za kishirikina (+Audio)

on

Golikipa mkongwe katika soka la Tanzania ambaye ana historia ya kucheza vilabu kadhaa Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania Ivo Mapunda  amekuwa na tabia ya kuingia uwanjani na taulo jeupe ambalo tumewahi kuliona mara kadhaa likileta hali ya sinto fahamu kwa wachezaji wa timu pinzani na hata muamuzi wakati mwingine.

DSC_8442

Ivo amekuwa na utamaduni ambao kwetu ni mgeni kidogo kwani tumezoea kuona makipa wa Ulaya pekee ndio watu ambao huwa wanaingia na taulo uwanjani kwa ajili ya kujifutia jasho, ugeni wa kitendo hicho kimekuwa kikileta utata kwa wachezaji timu pinzani wakiamini kwani hawafungi goli kutokana na uwepo wa taulo la Ivo nyavuni.

taulo

Team ya millardayo.com ilipata nafasi ya kufanya exclusive interview na kipa huyo ambaye utamaduni wa kutumia taulo jeupe wakati wa mechi amekuja nao wakati akitokea Kenya, ni kwa nini Ivo anatumia taulo jeupe? linaongeza chochote kuweza kumsaidia asifungwe

“Taulo halihusiani hata kidogo na mimi kuweza kucheza vizuri au kucheza vibaya uwanjani, taulo ni kitu ambacho magolikipa ulaya hutumia wakati wanapojifuta jasho au mvua kunyesha, ila kwa hapa wamekuwa na imani potofu kwa watu hata nilipokuwa Kenya ila mimi baada ya kuona wachezaji pinzani wanaathirika kisaikolojia ndio maana nalitumia”>>> Ivo Mapunda

Zaidi msikilize hapa

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments