AyoTV

A-Z:Mzee aliyekwenda na kipande cha gazeti Hospitali ya Muhimbili ili atibiwe haraka

on

Leo November 14, 2018 tunayo story kutokea kwa Mzee Alphonce Said ambaye amekwenda na kipande cha Gazeti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kitengo cha Mloganzila ili aweze kupatiwa matibabu kwa haraka.

Akizungumza na Ayo Tv, Mzee Said amesema alikwenda hospitalini hapo baada ya kusoma kwenye gazeti na kuona kuna taarifa kuhusu watu kupimwa bure afya zao katika hospitali hiyo, ambapo aliamua kwenda na gazeti lake kama ushahidi.

Mzee Said amesema baada ya kufika hospitalini hapo na gazeti hilo alipata faraja baada ya kupokelewa ambapo alipelekwa kupimwa afya yake na tayari anasubiri kufanyiwa matibabu.

“Madereva wa serikali nawapiga Pingu, mahakamani, tunawaondolea sifa”-Kamanda Muslim

Soma na hizi

Tupia Comments