Siku ya Leo limefanyika kongamano la sanaa ni pesa kongamano ambalo lengo lake kuu ni kuwafundisha wasanii namna nzuri ya kutunza pesa ili kuendana na hadhi yao sio tu kuwa na Majina makubwa bila pesa.
Wakati kongamano hilo likiendelea mgeni rasmi Hamis Mwinjuma naibu Waziri wa utamaduni sanaa na michezo akiwahutubia wasanii waliohudhuria amesema kuwa kuna pesa ilitolewa na Rais Samia kwaajili ya mikopo kwa wasanii lakini badala yake wasanii hao wengine walitumia kwenda kuonesha watu kuwa wao ni brand n.k
“Tulikua na matatizo hapa ndugu zangu waliokota wakaenda kutetea hadhi ya kuwa wasanii wakubwa mitaani kukawa na matatizo kwenye kurudisha, Tayari tumetengeneza utaratibu wa kuhakikisha pesa zile zinarudi maana zile pesa sio za ruzuku wala zawadi ila Fedha zile zilikua ni mikopo na lazima kila senti irudi, Tutaangalia namna rahisi ya kurudisha na kudaiana bila kudhalilishana ila lazima zirudi kwa njia yoyote ya kiserikali au kimtaani lazima pesa zirudi” Mwana FA