Top Stories

UPDATES: Ni kuhusu Sheikh Ponda mikononi mwa Polisi

on

Ni habari kutoka Kituo cha Polisi Kati Dar es salaam ambako Katibu Mkuu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda alikamatwa na kushikiliwa hapo.

Taarifa za jioni hii zimeeleza kwamba Ponda anaendelea kushikiliwa na Polisi mpaka sasa baada ya kukosa dhamana ikiwa ni siku moja tangu alipojisalimisha kwenye kituo hicho.

Akizungumza na millardayo.com na AyoTV, Wakili wa Sheikh Ponda, Juma Nassoro amesema Polisi wanaendelea kumshikilia na bado mpaka jioni hii hawajampatia masharti ya dhamana na vilevile jana October 13 saa 1 usiku Polisi walikwenda kupekua nyumbani kwake.

Pia Wakili Nassoro amesema kuwa miongoni kwa sababu za kukosa dhamana huenda ikawa ni maadhimisho ya kumbukumbu za kifo cha Mwalimu Nyerere ambapo ofisi nyingi za Serikali hazifanyi kazi.

October 12 Polisi ilitangaza kumpa siku 3 Sheikh Ponda kujisalimisha >>> ‘Ametenda makosa ya jinai kama uchochezi na kutoa lugha ambazo ni za kejeli dhifi ya serikali, ajisalimishe….. kukimbia hakutamsaidia” unaweza kutazama zaidi kwenye hii video hapa chini

Ulipitwa na hii? Wahujumu uchumi wafikishwa Mahakamani Kisutu leo

Soma na hizi

Tupia Comments