Michezo

Goodnews: mwanasoka mwenye asili ya Kenya aliesajiliwa Liverpool (pichaz na video)

on

Screen Shot 2014-07-30 at 3.35.54 AMBaada ya juzi usiku kukamilisha usajili wa Dejan Lovren, Liverpool imeendelea kujiimarisha kwa kufanya usajili mwingine ambao umemuhusisha staa alieng’aa kwenye kombe la dunia 2014 akiwa na timu ya taifa ya Ubelgiji.

Divock Origi mwenye asili ya Kenya ndio mchezaji mpya aliyejiunga na kikosi cha Brendan Rogers akitokea Lille ya Ufaransa kwa ada ya uhamisho wa £10m ambapo hata hivyo kwa mujibu wa BBC, Divock Origi ataendelea kuwepo Lille kwa mkopo hadi 2015 atakapojiunga rasmi na Liverpool.

Origi (19) ambae ni mtoto wa Mike Okoth aliyewahi kuwa mchezaji wa timu ya taifa ya Kenya (Harambee stars) amesaini mkataba wa miaka mitano lakini atabakia Lille kwa mkopo wa mwaka mmoja na atahamia Anfield msimu ujao.

Screen Shot 2014-07-30 at 3.19.05 AMBaba wa Origi akiongea na millardayo.com Kenya wiki iliyopita, alisema mwanae alianza soka toka akiwa mdogo na hakuona tatizo ndio maana alimruhusu afanye anachopenda ambapo kwenye sentensi nyingine Baba anasema tofauti na wengine wanavyoweza kudhani, Origi ni mzungumzaji wa lugha ya Kiswahili pia.

Kama unahitaji kuona Divock akiwa uwanjani inakuaje, unaweza kuitazama hii video yake hapa chini

Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>> twitter Insta FB

Tupia Comments