Top Stories

Kilichoikwamisha Mahakama kesi ya Mhasibu TAKUKURU hiki hapa (+video)

on

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeshindwa kusikiliza ushahidi wa kesi inayomkabili aliyekuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru, Godfrey Gugai kwa sababu mashahidi hawana nauli.

Hayo yameelezwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Awamu Mbagwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kuanza kusikilizwa.

Wakili Mbagwa amesema mashahidi wameshindwa kufika kwa sababu wa mpangilio wa Kiutawala ambapo mashahidi hawana nauli na utawala hautoi nauli hadi mashahidi wafike.

Tunasikitika kwamba hatuwezi kuendelea na kesi hii, tunaomba ahirisho ili kuangalia utawala umefikia wapi, amesema.

Hakimu Simba amesema hilo suala halina tatizo linazungumzika na kutatulika ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi Aprili 8, 2019.

Gugai ambaye alikuwa Mhasibu Mkuu wa Takukuru na wenzake watatu wanakabiliwa na kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizolingana na kipato chake halali.

MPEMBA ANAEFANYA HIPHOP… “CHUGA KITU GANI NIMEVUKA MAJI” HAIKUANZIA MWANZA WALA ARUSHA

Soma na hizi

Tupia Comments