Michezo

Kocha wa Tottenham Mauricio Pochettino amefungiwa leo

on

Kocha wa club ya Tottenham Hotspurs ya England Mauricio Pochettino amekutana na rungu la chama cha soka England FA kutokana na kitendo chake cha kumfokea refa Mike Dean wakati wa mchezo kati ya Tottenham Hotspurs dhidi ya Burnley uliyomalizika kwa Spurs kupoteza kwa magoli 2-1.

Game hiyo iliyochezwa February 23 na kumalizika Mauricio Pochettino akimlaumu refa Mike Dean, hata hivyo baada ya tukio hilo kutokea Mauricio Pochettino alikiri kosa na kuomba radhi ila chama cha soka England FA kimeamuadhibu Mauricio Pochettino kwa kumfungia mechi mbili kukaa kwenye benchi.

Hata hivyo tofauti kati ya Mike Dean na Pochettino ilipelekea bodi ya waamuzi imetangaza kuwa Mike Dean atakuwa muamuzi wa akiba wa mchezo wa Man City dhidi ya West Ham United na kumuondoka katika mchezo kati ya Spurs dhidi ya Chelsea uliochezwa katika uwanja wa  Stamford Bridge.

Mwinyi Zahera alisababisha shabiki wa Yanga abet mke wake

Soma na hizi

Tupia Comments