Michezo

Cristiano Ronaldo apata majeraha, hofu yatanda kwa mashabiki wa Juventus

on

Staa wa kimataifa wa Ureno anayeichezea club ya Juventus ya Italia Cristiano Ronaldo ameripotiwa kuwa ameumia misuli wakati akiitumikia timu yake ya taifa ya Ureno katika mchezo wa kuwania kucheza fainali za mataifa ya Ulaya (Euro 2020) dhidi ya Serbia.

Ronaldo alilazimika kutolewa nje ya uwanja dakika ya 31 ya mchezo kufuatia kuumia kwake misuli, wakati ambao timu yake ikiwa nyuma kwa goli 1-0 lililokuwa limefungwa na Dusan Tadic dakika ya 7 ya mchezo, pamoja na Ureno kumkosa Ronaldo walifanikiwa kusawazisha dakika ya 42 kupitia kwa Pereira na game kumalizika kwa sare ya 1-1.

Cristiano Ronaldo ambaye mwenye alisema anajijua kwa jeraha alilopata hawezi kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya wiki moja au mbili, aliumia wakati akijaribu kukimbilia pasi ndefu aliyokuwa amepigiwa kwa mbali, bado haijatoka taarifa rasmi kama Ronaldo atakuwa nje ya uwanja kwa muda gani ila mashabiki wa Juventus wameanza kuwa na hofu kuwa wanaweza kumkosa katika mchezo wa robo fainali ya UEFA Champions League.

MUHIMBILI JKCI NAO WATANGAZA NUSU BEI KWA USHINDI WA TAIFA STARS

Soma na hizi

Tupia Comments