Club ya FC Barcelona leo saa 23:00 EAT itacheza game yake ya nusu fainali ya michuano ya Copa Del Rey dhidi ya wapinzani wao Real Madrid, game inayokutanisha timu dhidi yao kwa kawaida imepewa jina El Clasico nchini Hispania.
Leo katika game hiyo ya nusu fainali FC Barcelona watavaa jezi zilizoandikwa majina yao kwa lugha mbili lugha ya kawaida tuliyoizoea lakini pia yatakuwa yametafsiriwa kichina, lengo likiwa ni kusherehekea mwaka mpya wa China kwa kuonesha mapenzi kwa mashabiki wao wa China au kukuza zaidi wigo wa mashabiki.
Kila mwaka taifa la China huwa na utamaduni wa kusherehekea mwaka wake mpya wa kichina na mwaka huu imeangukia February 5 2019, ndio maana Barcelona wamefanya hivyo kuonesha mapenzi yao kwao, kwa kawaida mwaka mpya wa China huwa unaangukia kati ya January 21 hadi February 20.
Michael Wambura sasa kumpeleka Mahakamani Wallace Karia wa TFF