Habari za Mastaa

Ommy Dimpoz afanya balaa GSM Mall, mashabiki hawajaamini “Nilitetereka”(+video)

on

Msanii anayetamba na ngoma ya ‘You Are The BestOmmy Dimpoz leo amekamata headline nyingine baada ya kuwapigisha pamba mashabiki zake wawili katika duka la GSM MALL Pugu ikiwa ni muendelezo wa kutoa zawadi kwa mashabiki zake.

Dimpoz ametoa zawadi hizo baada ya kuchagua mashabiki hao mmoja akiwa wa Kike na mmoja wa Kiume kupitia akaunti yake ya Instagram ambapo kutokana na mchango wao katika kazi zake.

Akizungumza na waandishi wa habari, Dimpoz amesema huo ni muendelezo na atafanya hivyo kwa mashabiki wanaosapoti kazi zake na pengine kifurushi cha zawadi anazozitoa kinaweza kubadilika kulingana na mfuko wake kwani anaweza kutoa gari.

Umati wa watu ulivyojitokeza kumshuhudia Rais Magufuli akiizindua Barabara Mbinga

Soma na hizi

Tupia Comments