AyoTV

Mwanzo Mwisho: Waziri Ummy alivyombananisha Muuza Viwanja, akamatwa kikaoni(+video)

on

Tunayo story kutokea kwa Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu ambapo ameagiza kuchukuliwa hatua kwa Mzee Seif Bahari anayedaiwa kuuza maeneo ya Kituo cha Wazee wa Ukoma Nunge Kigamboni.

Waziri Mwalimu ametoa agizo hilo baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa mmoja wa waathirika wa ugonjwa wa Ukoma katika kituo hicho, Mzee Salum Ubwabwa wakati alipokuwa akizungumza nao kuhusu maadhimisho ya ugonjwa huo yanayotarajiwa kufanyika January 27, 2019.

“Tumfatilie na tumchukulie hatua kuhusu maeneo hayo aliyoyauza, huyu ndio anauza maeneo haya na kama anataka kuuza si akauze kwake,”amesema.

MSICHANA ALIYEONGOZA KITAIFA AMUANGUKIA MAGUFULI “TUSIUWE VIPAJI”

Soma na hizi

Tupia Comments