Leo October 30, 2018 tunayo story kuhusu matumizi ya nembo za RED CROSS, ambapo Katibu Mkuu wa RED CROSS nchini Tanzania, Julius Kejo amesema sio kila Ambulance inapaswa kutumia nembo ya Msalaba Mwekundu.
Kejo amesema Red Cross inatoa huduma bure na haipendeleo, hivyo wanaopaswa kutumia nembo hizo ni watu wanaotoa huduma za Kibinadaamu ambapo pia sheria za Kimataifa zinatoa kibali cha kutumia nembo hizo kwa vikosi vya tiba za Kijeshi.
Amesema mchakato unaendelea wa kuihusha sheria ya Red Cross na adhabu sahihi zinazoweza kutolewa kuhusu matumizi yasio sahihi kuhusu nembo hizo.