Mwigizaji nguli kutoka Bara la Asia, Jackie Chan (67) amefunguka kuwa atatoa sehemu ya utajiri wake unaofikia Dola za Marekani 370 milioni (takriban Sh 850 bilioni) kwa watu wenye uhitaji kuliko kumpa mwanawe wa kiume, Jaycee.
Alipokuwa akihojiwa na NewAsia, Chan alitoa maelezo kuwa ameamua kutompa urithi huo wa utajiri Jaycee (39) kwa kigezo kuwa kama mwanae ana uwezo wa kutafuta, ni heri akatafuta pesa zake mwenyewe.
Jaycee ni mtoto pekee wa Chan na mkewe, Joan Lin waliooana mwaka 1982. Jay ni muigizaji na pia ni mwanamuziki. Mwaka 2014 aliwahi kukamatwa na dawa za kulevya na Chan alitumia nguvu kubwa kuomba radhi mbele ya umma kuhusiana na hilo.