Stori Kubwa

Kuna kingine kipya kuhusu mtoto wa Jackie Chain

on

cd97d23290964049b541dcc0411ea260

Jaycee akiwa Mahakamani China mwezi January, 2015

Kitendo cha mtoto wa mwigizaji maarufu China, Jackie Chan aitwaye Jaycee Chan kukamatwa na dawa za kulevya nyumbani kwake kilimfedhehesha sana baba yake sio tu kwa sababu ya umaarufu wake, bali heshima yake pia kama balozi wa mapambano ya dawa za kulevya ndani ya China.

Jaycee Chan baada ya kutumikia kifungo cha miezi sita jela katika gereza la Checheng kwa kosa la kukutwa na dawa za kulevya nyumbani kwake, kwa sasa yuko huru huku kukiwa na taarifa kwamba atazungumza na waandishi wa Habari muda wowote kuanzia sasa.

1408454619_jackie-jaycee-chan-zoom

Jackie Chan akiwa na mtoto wake

Polisi walimkamata mtoto wa Jackie Chan Agosti mwaka jana pamoja na mwenzake Ko Chen katika nyumba yake iliyopo Beijing, China baada ya kukutwa na zaidi ya gramu 100 za bangi.

Chan anakuwa staa mkubwa kwa China kukutwa na kiwango kikubwa cha dawa za kulevya kwa mwaka 2014, angeweza kutumikia adhabu hiyo miaka mingi zaidi lakini mahakama ilipunguza adhabu baada ya kukiri kufanya kosa hilo.

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments