Premier Bet SwahiliFlix Ad Tigo Ad

Top Stories

Jaji aamuru Trump arudishe Bilioni 4 alizotumia

on

Leo November 8, 2019 Jaji wa Jimbo la New York ameamuru Rais Donald Trump azirudishe Dola milioni 2 zaidi ya Tsh. Bilioni 4 alizozichukua kwa matumizi yanayotajwa na Mahakama kuwa ni kinyume cha sheria.

Inadaiwa alichukua Fedha hizo kutoka katika Mfuko wa Misaada wa ‘Trump Foundation’ na kuzitumia katika kampeni zake kwenye uchaguzi wa mwaka 2016 uliomuingiza madarakani.

Uamuzi huu ni sehemu ya mashitaka yaliyowasilishwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Jimbo la New York dhidi ya Mfuko wa Misaada wa ‘Donald J Trump Foundation’ akiwemo Rais mwenyewe na watoto wake, Donald Junior, Ivanka na Eric.

Mahakama pia, imeelekeza watoto wa Rais Trump wanaosimamia mfuko huo kupatiwa mafunzo ya lazima kuhusu uongozi na kujua namna ya kufanya maamuzi ya matumizi ya fedha kwa misingi ya kisheria.

HIZI NDIZO TIMU MBILI KUBWA ZA LIGI KUU YA UINGEREZA ZINAZOMTAKA SAMATTA

Soma na hizi

Tupia Comments