Jaji Tanya Chutkan meiidhinisha pendekezo la mwendesha mashtaka maalum Jack Smith, ambaye anaendesha kesi dhidi ya Donald Trump kwa majaribio haramu ya kutengua matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2020, kusitisha mashtaka kwa msingi kwamba sasa ndiye rais mteule.
Ombi la Jack Smith la kusitishwa kwa mashtaka ya shirikisho kwa kushikilia hati zilizoainishwa bado halijashughulikiwa.
Katika maamuzi yake mawili, mwendesha mashtaka maalum Jack Smith hivyo anakubaliana na sera iliyopitishwa zaidi ya miaka 50 iliyopita na Wizara ya Sheria, inayojumuisha kutomshtaki rais aliye madarakani.
Lakini amemtaka jaji kumaliza kesi hiyo bila kuhukumu mapema mwenendo wa matukio, jambo ambalo linaacha wazi uwezekano kwamba kesi hizi zinaweza kufunguliwa tena mwishoni mwa mamlaka ya Donald Trump.
Dakika chache baadaye, Jack Smith pia ametangaza kwamba anasitisha kumfuatilia Donald Trump kwa kushikilia hati za siri baada ya kuondoka kwake kutoka Ikulu ya White House mnamo mwaka 2021.
Mwendesha mashtaka maalum pia anachunguza kesi hii dhidi ya Donald Trump.
Jack Smith amekata rufaa dhidi ya uamuzi wa jaji wa shirikisho Aileen Cannon huko Florida. Uamuzi huu ulifuta utaratibu huo mwezi Julai kwa madai kuwa uteuzi wa mwendesha mashtaka maalum katika kesi hii ulikuwa kinyume cha katiba. Sasa anakataa rufaa hii.