Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma amewataka majaji kutumia zaidi teknolojia ya akili mnemba ili kuondokana na changamoto ya mlundikano wa mashauri kwa lengo la kuboresha ufanisi wa mfumo wa sheria na kupunguza mashauri katika mahakama.
Ameyasema hayo katika Mkutano wa nusu mwaka uliokutanisha majaji mbalimbali kutoka mahakama za Rufani Nchini kwa lengo kuboresha utendaji na kutatua changamoto zinanazoikabili sekta hiyo.
Aidha jaji Mkuu huyo amewataka majaji wa mahakama za Rufani kufanya mazoezi ili kuepukana na matatizo ya afya ya akili yanayosababishwa na kesi ngumu wanazokutana nazo mahakamani.
Hata hivyo Jaji Ibrahim ameongeza kuwa wanakutana na migogoro mbalimbali ikiwemo ya kikatiba, kiuchumi, kisiasa, na kijamii,ambayo imeshndwa kutafutiwa ufumbuzi ngazi za chini hivyo watafanya utafiti kisheria ili kupatiwa ufumbuzi zaidi kutokana na wao kupatiwa kesi hizo.
Jaji Mkuu ameendelea kusemakua Takwimu zinaonyesha kuwa, hadi kufikia Juni 2024,
Mahakama ya Rufani ilikuwa na mashauri 1,248ya mlundikano, yaani mashauri yanayozidi miezi 24.
Idadi hii ya mashauri kwa idadi ya majopo 11tuliyonayo ni kusema kuwa, kila jopo la majaji watatu wa Rufani lilikuwa na mzigo wa mashauri 113.
Amesema Uzoefu mkubwa, ujuzi wa kina, na Akili kubwa waliyonayo Majaji wa Rufani ni lazima yaboreshwe, yaendelezwe kwa kuyafuatilia matukio mbalimbali na mabadiliko makubwa ya sayansi na teknolojia, utandawazi na muingiliano wa mifumo mbalimbali ya kisheria kutoka sehemu mbalimbali duniani.
Kwa upande wake msajili wa Mahakama ya Rufani George Herbert amesema mpaka kufikia mwaka huu walikuwa na mashauri 5900 Hadi kufikia mwezi wa Sita yamesikilizwa 941 mashauri mengine yanasubiri kupatiwa vikao hivyo technolojia ya akili mnemba imekuja na utatuzi wa kutatua changamoto hizo.
Msajili ameendelea kusemakuwa technolojia hii itawasidia kupunguza kupunguza mashauri na malalamiko waliyokua nayo wananchi na upatikanaji ya maandiko mbalimbali katika rufaa na kupunguza muda wa usikizaji mashauri.