AyoTV

Kilichosababisha Jackline Wolper awaonye vijana kuhusu unywaji wa pombe

on

Kuna usemi unaosema kuwa ‘Wasanii ni kioo cha jamii’ ambapo wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha jamii inafuata maadili, leo April 3, 2017 nimeipata stori hii ya staa wa Bongo movies Jackline Wolper ambaye kupitia ukurasa wake wa Instagram aliwaonya vijana juu ya unywaji pombe.

Wolper alikwenda mbali zaidi na kuwashauri vijana ambao hawatumii pombe wajiepushe nayo ambapo kupitia  AyoTV Entertainment na millardayo.com, Jackline Wolper anatueleza sababu za kuandika hivyo.

>>“Niliandika kuhusu pombe kwa sababu naamini pombe labda ndiyo inaweza kuwa ilinifanya nikawa mnene kutokana na mwanzo mimi nilikuwa sinywi pombe kabisa na nilikuwa sijui kitu kinaitwa pombe na hata mtu alikuwa akinywa, mimi namshangaa kabisa. Kwa hiyo ndiyo nikaandika vile pombe siyo nzuri kwa wasichana ambao ndiyo wanaanza kujifunza pombe na wana miili yao mizuri tu. Waache kunywa pombe.” Jackline Wolper.

Bonyeza Play hapa kusikiliza alivyoongea Jackline Wolper>>>

 

Video:Nisingependa upitwe na vipaji nilivyokutana navyo kwenye maonyesho ya VAA AFRICA Arusha>>>

Soma na hizi

Tupia Comments