Mwanaume mmoja mwenye silaha ajiuwa kwa risasi baada ya kuwapiga risasi na kuwaua watu sita katika sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa ya mpenzi wake huko Colorado Springs nchini Marekani siku ya Jumapili, polisi wameeleza.
Milio ya risasi ilisikika katika bustani ya nyumbani ambapo familia ilikutana kusheherekea.
“Mwanaume ambaye ni mpenzi wa msichana aliyekuwa anasheherekea siku yake ya kuzaliwa, alifika nyumbani hapo na kuanza kupiga risasi watu waliokuwa katika sherehe hiyo kabla ya kujiua yeye mwenyewe” Idara ya Polisi ya Colorado Springs
Sababu ya shambulio hilo halijafahamika mpaka sasa. Watu wote waliopigwa risasi walikuwa watu wazima ingawa kulikuwa na watoto katika sherehe hiyo katika wakati huo.
Hawajatajwa majina watu waliopigwa risasi na hata mshambuliaji hajatajwa bado.
“Tukio la kikatili limepelekea watu sita kufariki na wengine kujeruhiwa. Watoto hawakujeruhiwa na mshukiwa huyo na wapo na ndugu zao sasa” Polisi