Mix

Unamkumbuka jamaa aliyekuwa mkalimani kwenye msiba wa Mandela?kapata dili hii.

on

jamaa2Ni jamaa ambaye dunia ilimtambua kwenye mazishi ya Hayati Mzee Nelson Mandela mwaka jana ambaye kazi yake ilikua ni kutafsiri lugha za ishara ambaye baadae aliinga kwa headline na vyombo mbalimbali vya habari baada ya kufahamika hakua akipatia lugha ile ya ishara.

Thamsanqa Jantjie ndiye jina lake ambapo dunia ilimkashifu na hasa walemavu kwa kutoa ishara zisizotafsirika kwa sasa amepata ajira baadae Jantjie alijitetea kuwa alishikwa na kiwewe na kuona mazingaombwe wakati wa maziko hayo.

jamaaJantjie kwa sasa ameonekana katika tangazo la biashara akikejeli tukio hilo lililompa umaarufu kote duniani katika tangazo hilo ambalo linapigia debe mtandao wa kijamii wa Livelens uliotengezwa na kampuni moja kutoka Tel Aviv Israili.

Afisa mkuu mtendaji wa kampuni hiyo Max Bluvbland ameiambia BBC kuwa Jantjie yuko timamu na kuwa alitekeleza majukumu yake bila tashwishi yeyote ”yeye ni mtu timamu aliyepatikana na mkasa anaojutia.

Source:Bbc.

 

Tupia Comments