Mix

Baada ya Diamond na Alikiba, Dogo Janja naye kuleta bidhaa zenye jina lake

on

Mwimbaji staa anayetamba na wimbo wa ‘Ukivaaje unapendeza?’ Dogo Janjaamefunguka akisema sasa ana mpango wa kufanya biashara akitumia Brand yake ya Dogo Janja akidai ataingiza sokoni bidhaa tofauti na nguo.

Akizungumza kwenye 255 ya XXL ya Clouds FM Dogo Janja amesema ataingiza sokoni bidhaa zinazowahusu watoto zaidi akidai kuwa na mpango wa kuleta vifaa vya michezo kwa watoto kama game ya Dogo Janja.

>>“Brand ya Dogo Janja itakuja lakini mimi sitakuja na Brand ya nguo ila nitakuja na vifaa vya watoto vya michezo vya Dogo Janja. Mimi nitakuwa na-deal na madogo janja zaidi. Hii ipo kama mwezi wa Sita nadhani Mungu akijaalia nitasafiri kwenda kufanya mitikasi. Kwa hiyo, nikirudi narudi na bidhaa.” – Dogo Janja

VIDEO: Diamond alivyoizindua Chibu Perfume

Ulipitwa: Diamond Platnumz alivyo perfom kwenye Tamasha Nairobi (+video)

Soma na hizi

Tupia Comments