Bunge la nchini Japan limemfukuza bungeni mbunge mmoja ambaye pia ni mwanablogu wa YouTube kwa kutohudhuria vikao vya bunge kwa muda mrefu.
Kulingana na jarida la AFP, hii ni mara ya kwanza kwa bunge la taifa hilo la bara Asia kufanya hivyo kwa Zaidi ya miaka 70 iliyopita.
Yoshikazu Higashitani, anayejulikana kwa jina lake la mtandaoni kama GaaSyy, alikuwa ameagizwa kuomba msamaha kwa kutokuwepo kwake kwa miezi kadhaa mapema Machi.
Lakini mbunge huyo, mmoja wa wanachama wawili waliochaguliwa wa chama pinzani Seijika Joshi 48, hakuhudhuria kikao hicho cha bunge pia.
Higashitani, 51, hakuhudhuria katika Baraza la Madiwani tangu uchaguzi wake wa Julai 2022, licha ya hitaji la wabunge kuwepo.
Baraza la Upper House la Japan liliamua Jumanne kumfukuza kutoka bungeni.
Hatua hiyo ilifanywa rasmi Jumatano na kumfanya kuwa mbunge wa kwanza wa Kijapani kufukuzwa tangu 1951, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.
Nafasi ya Higashitani itachukuliwa na mwanachama mwingine wa chama chake.