Japan inachukua mipango ya hatua kuelekea kufanya maisha ya Mwezi kuwa ukweli,ambapo Chuo Kikuu cha Kyoto na kampuni kubwa ya ujenzi ya Kajima Corp wakishirikiana kuunda makazi ya mwezi ambayo hutoa mvuto bandia, vyombo vya habari vya ndani viliripoti Jumapili.
Mradi wa “Neo Lunar Glass” unalenga kuunda muundo wa paraboloid wenye uwezo wa kuiga hali zinazofanana na Dunia kwa kutumia mzunguko ili kuzalisha mvuto na mpango huo unatarajiwa kukamilika ifikapo miaka ya 2030, kulingana na Kyodo News.
“Mradi huu unahitaji kasi kubwa ya kiteknolojia, lakini tunalenga kuufanikisha na kuweka njia kwenye anga,” alisema Yosuke Yamashiki, profesa wa masomo ya juu jumuishi ya kuishi kwa binadamu katika Chuo Kikuu cha Kyoto.
Muundo wa Lunar Glass utakuwa na kipenyo cha takriban mita 200 na urefu wa mita 400, wenye uwezo wa kukaa hadi watu 10,000, kulingana na shirika hilo.
Mradi huo unatarajiwa kuzinduliwa katika mwaka huu wa fedha